Ndalichako “Maria na Consolata ni Mashujaa wa Taifa”

Ndalichako “Maria na Consolata ni Mashujaa wa Taifa”
"Ni mashujaa wa taifa letu" hiki ndicho alichosema Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya pacha walioungana, Maria na Consolata Mwakikuti.

Akizungumza leo Juni 5 mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya pacha hao, Profesa Ndalichako amesema mashujaa hao wameliacha taifa katika simanzi nzito.

"Mara ya mwisho niliwaona pale Mwaisela wakiwa wodi ya wagonjwa mahututi, inaniumiza mno lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe," amesema.

Amesema wizara hiyo imepoteza watu muhimu waliokuwa wakipigania elimu bila kujali ulemavu na namna walivyo.

“Lakini kubwa wametufundisha umoja na upendo. Wamekuwa pamoja kwa miaka 21," amesema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad