Saratani ni ugonjwa ambao unaweza kuathiri kiungo chochote cha mwili, ikiwa utapata matibabu haraka, unaweza kupona, lakini ukikawia bila kupata matibabu, husababisha kifo, ni ugonjwa unaosababisha vifo vingi kutokana na gharama za matibabu.
Saratani ni ugonjwa usiokuwa wa kuambukiza lakini unaweza kurithi kutokana na vinasaba, akizungumza na Eatv Dkt. Sarah Maongezi kutoka kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambikiza, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto amezitaja saratani ya matiti kwa akina mama pamoja saratani tezi dume kwa wanaume.
"Saratani haiambukizwi lakini unaweza kurithi na zinazoweza kurithika ni zile zinazotokana na vinasaba pekee ambazo ni saratani ya matiti kwa wakina mama na tezi tume kwa wakina baba”, amesema Dkt. Maongezi.
Saratani nyingine za kawaida ambazo huwaathiri wanaume kwa wanawake ni saratani ya mapafu, utumbo, maini, mdomo na ngozi.