Nilichomewa Nyumba Yangu Moto, Nilimpoteza Baba Lakini kwa Hili Sitakubali – Hawa Ghasia

Nilichomewa Nyumba Yangu Moto, Nilimpoteza Baba Lakini kwa Hili Sitakubali – Hawa Ghasia
Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasia amesema kuwa wakati wa sakata la gesi alikaa upande wa serikali kuitetea kupeleka gesi kokote Tanzania aliamini inatenda haki lakini badala yake nyumba yake ilichomwa na alimpoteza baba yake.



Ghasia ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akichangia hoja ya bajeti ya serikali ambapo amesema kwa hili la korosho hawezi kubaliani na mapendekezo ya serikali kufuta asilimia 65 ya fedha zinazotokana na mauzo ya korosho.

“Kwanza nianze kwa masikitiko makubwa sana ambayo yanasambazwa kwa makusudi dhidi ya Wabunge wanaotetea kupelekewa pembejeo Kwenye maeneo yao.Tuna taarifa jana watu wamekaa vikao waje humu kutudhalilisha Wabunge tunaowatetea wananchi wetu wapate pembejeo,” amesema Hawa.

“Wabunge wote humu ndani tuna haki sawa za kutetea wananchi wetu. Anayetoka Kwenye pamba ataitetea pamba, anayetoka Kwenye madini atatetea madini yake, anayetoka Kwenye korosho ana haki ya kuitetea korosho yake.Mimi napenda niwahakikishie wananchi wanaolima korosho; Wabunge wao tupo imara, tutapambana kuhakikisha haki hii inapatikana. Hata kama haitapatikana, wajibu wetu tutautimiza kama wawakilishi kuja kuwatetea wananchi,” ameongeza

“Mimi nilikaa upande wa serikali wakati wa gesi. Niliitetea Serikali kupeleka gesi kokote Tanzania kwa sababu nilijua serikali inafanya haki. Nilichomewa nyumba yangu moto. Mabomba ya kupeleka maji Kijijini kwetu yaling’olewa. Mikorosho ya Baba yangu ilikatwa. Minazi ya Baba yangu ilikatwa. Katika process hiyo nilipoteza Baba yangu. Bado nilimshukuru Mwenyezi Mungu nilisema Alhamdulilah Alhamdullilah Alhamdulillah! Kwa sababu niliona serikali inachokifanya iko sahihi,” alisisitiza Ghasia.

“Ninachosema kama kuna mtu amefanya ubadhilifu, hata kama ni Hawa Ghasia Kwenye mfuko wa korosho, nipelekeni Mahakamani.Hao wananchi tunaowambia wabunge wa Kusini wabinafsi wanataka kuigawa nchi wana akili na wanajiongeza.”
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad