STAA wa filamu na muziki Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amefunguka jinsi alivyoteswa na penzi la mwanaume mwenye umri mdogo ‘kibenteni’ kutokana na kumgeuza ‘ATM’ kwa kumuhudumia kama mwanaye.
Nisha aliiambia Za Motomoto News kuwa wakati akiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kibenteni huyo ambaye hakutaka kumtaja jina alikuwa akimnunulia kila kitu na kumpa fedha na kumuhudumia kama mtoto wake lakini baadaye alikuja kushtuka kuwa anachunwa na kuamua kuachana naye.
“Nimejifunza sana na nimekoma kuwa na uhusiano na mwanaume ninayemzidi umri na kipato maana nilijikuta nimeingia kwenye uhusiano huo bila kujua kwamba kibenteni huyo ni tegemezi ambaye alinifanya kama mashine yake ya ATM na kunikomoa kuja kushtuka ameshanikwangua vya kutosha,” alisema Nisha.
Hata hivyo Nisha aliwataka mastaa wa kike kuwa makini wanapoingia kwenye uhusiano kwani kwa sasa kuna wanaume vibenteni ambao wanatafuta wanawake wanaowazidi kipato na umri wakiwa na dhumuni la kuwachuna fedha zao.
Chanzo: Global Publishers