Ntazaa Mtoto Mwingine Mapema Iwezekanavyo- Aika

Ntazaa Mtoto Mwingine Mapema Iwezekanavyo- Aika
Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni mmoja wa memba wa kundi la Navy Kenzo, Aika Mareale amesema kwa kuwa mtoto wake wa kwanza Gold, aliyezaa na memba mwenzake Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ ndio amemfungulia njia na sasa atamleta mtoto mwingine mapema iwezekanavyo.


Akizungumza na eatv.tv Aika amesema kuwa, amezaa mtoto mmoja na ameona raha kuwa mama hivyo basi hana muda wa kujishauri tena bali ni kumleta mdogo wa Gold mapema wala sio muda wa kupoteza hivi sasa na kukaa miaka mitatu au minne ndio kuzaa mtoto mwingine.

“Najisikia furaha sana kuwa mama hata wa watoto watano hivi nimeona raha ya kuzaa na hivi sasa niko njiani kuleta mtoto mwingine mambo ya kupishana muda mrefu sio sawa kabisa,” amesema Aika.

Pia ameongeza kuwa kusema alikuwa kwenye mahusiano muda mrefu na nahreel bila kuzaa ,alichelewa hivyo kwakua walikuwa wanasubiria muda mwafaka ufike na muda huo umefika.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad