Paka Atabiri Mshindi Mechi ya Ufunguzi Kombe la Dunia

Paka Atabiri Mshindi Mechi ya Ufunguzi Kombe la Dunia
Paka mmoja maarufu ambaye anadaiwa kuwa na uwezo wa kipekee wa kutabiri ametabiri mshindi wa mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia nchini Urusi.


Kwa mujibu wa paka huyo aliyepewa jina Achilles, Urusi ndio watakaoshinda mechi hiyo, Achilles ni paka wa rangi nyeupe ambaye ni kiziwi, hubashiri mshindi kwa kuchagua katika ya bakuli mbili ambazo zimewekwa bendera za mataifa yanayocheza.

Paka huyo ni miongoni mwa paka wanaofugwa kukabiliana na panya katika makumbusho ya Hermitage mjini St Petersburg, ingawa sasa ana majukumu hayo mapya.

"Achilles yuko tayari kutumiwa kwa umma na huwa hana wasiwasi kuwa eneo lenye watu wengi," amesema daktari wa mifugo Anna Kondratyeva, ambaye humtunza.

Paka huyo anafuata katika nyayo za Paul the Octopus, pweza aliyepata umaarufu baada ya kutabiri mshindi wa mechi za Kombe la Dunia mwaka 2010, michuano iliyoandaliwa nchini Afrika Kusini.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad