Ni baada ya Mafundi waliofika kuukarabati mtambo huo wa ATM ambao ulikuwa umeharibika kwa siku 12 katika jimbo moja nchini India walipigwa na butwaa walipoufungua kubaini tatizo lilikuwa wapi.
Noti za thamani ya rupia 1.2m (£13,300; $17,600) zilikuwa zimechanwa na kuraruliwa na panya katika benki hiyo jimbo la Assam.
Polisi wanasema panya hao pengine waliingia ndani ya mtambo huo kwa kupitia kwenye tundu lililokuwa litumiwe kuingizia nyaya, gazeti la Hindustan Times limeripoti.
Mafundi waliofungua mtambo huo walipata noti za rupia 2,000 na rupia 500 zikiwa zimeharibiwa.
Walifanikiwa kunusuru noti za jumla ya thamani ya rupia 1.7 milioni.