“Pesa Haiishi Utamu” - Kitwanga

“Pesa haiishi utamu” - Kitwanga
Mbunge wa Misungwi (CCM) Charles Kitwanga, amewataka wananchi na wabunge kutoshangaa serikali kudaiwa madeni, kwasababu pesa inatabia ya kutotosheleza mahitaji yote  na vilevile pesa haiwezi kuisha matumizi yake.


Kitwanga amesema hayo leo Juni 18, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, alipokuwa akichangia hoja mjadala wa mapendekezo ya Bajeti kuu ya Serikali katika mwaka wa fedha 2018/2019 na kusema kuwa Bajeti hiyo imetimiza viwango vya kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda.

“Tabia ya pesa zipo mbili, kwanza pesa huwa hazitoshi, pili pesa huwa haiishi utamu kwahiyo ndugu zangu wa mkono wangu wa kulia, kilasiku wanapokuwa wanalalamika kwamba tuna madeni ni kwasababu pesa siku zote huwa haitoshi na utamu hauishi” amesema Kitwanga

Kitwanga ameongeza kuwa, mapendekezo hayo ya Bajeti yamelenga katika mpango wa maendeleo 2025 kwa kufikia uchumi wa kati na kuitaka Serikali kuondoa vikwazo, ikiwemo kutumia muda mrefu wa kupewa leseni kwa watu wenye lengo la kuanzisha viwanda nchini.

Bunge kwasasa linajadili mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali kuu katika mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo Serikali imepanga kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 32.4 ya kugharamia miradi ya maendeleo na mahitaji ya kawaida.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad