Polepole amesema hayo ikiwa zimepita siku kadhaa baada ya mazishi ya Mwl. Kasuku Bilago kuzikwa huko Kakonko mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mfupi na kisha kwenda kuzikwa huko kijijini kwao.
Polepole amesema kuwa "Nimesikia jamaa palepale msibani walianza kugawana ubunge na kuanza kujihadaa, ni bahati mbaya sana. Utamaduni wa kiafrika ni kumaliza msiba ambapo lengo ni kufariji wafiwa".
Ameongeza kuwa "Nimekaa Kakonko kwa muda wa kutosha, kwakuwa mmeanza siasa msibani, CCM tunasema wembe ni uleule".
Wakiwa kwenye mazishi ya Mwalimu Bilago ambaye alikuwa Mbunge kupitia CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Mbowe walikubaliana kuweka umoja ambao utamsimamisha mgombea mmoja anayekubalika kutoka upinzani na kuhakikishia wanampigania hadi anashinda ili kumuenzi mwalimu