Polisi Yakanusha Kuhusu Taarifa za Muuguzi Kuuliwa na Askari

Polisi Yakanusha Kuhusu Taarifa za Muuguzi Kuuliwa na Askari
Yakiwa yamepita masaa machache tokea zilipovuma tetesi za mauji ya muuguzi mmoja mkoani Mwanza dhidi ya askari Polisi mkoani humo, Jeshi la Polisi limefunguka na kukanusha taarifa hizo huku wakiwataka waandishi wa habari kuacha kuandika vitu kwa mihemuko bila ya kufuata utaratibu.


Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi wakati alipokuwa anazungumzia juu ya tukio hilo na kusema kwamba mnamo Juni 09, 2018 majira ya saa 5:00 usiku katika mtaa wa Misungwi ambapo kikundi cha walinzi walimkamata mwananchi ambaye alifahamika jina la Christian Audock Joseph wakiwa wanamtuhumu kwa kosa la wizi katika maduka waliyokuwa wanayalinda.

Msikilize hapa chini Kamanda Ahmed Msangi akielezea tukio zima jinsi lilivyotokea mpaka muuguzi huyo kufariki dunia na kupelekea askari wa Jeshi la Polisi kutuhumiwa na mauaji hayo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad