Producer Nahreel Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Kuhusu Rosa Ree Kusainiwa na Lebo ya South Africa


#GetToKnow Mapema mwezi uliopita, The female rapper Rosa Ree alimwaga wino na kuthibitisha rasmi kusaini dili nono na lebo ya 'DIMO PRODUCTION' yenye makazi yake nchini Afrika Kusini.

Sasa kwa mara ya kwanza tangu mchongo huo ufanyike, Nahreel ambaye ni Meneja wa zamani wa rapper huyo chini ya The Industry Label, ametuchana maoni yake juu ya ishu hiyo ukizingatia wao ndio waliomtoa from the bottom.
-
"Mimi nadhani tulichokifanya tumekifanya kwa uwezo wetu, tumeweza kutengeneza kitu ambacho kiliweza kuonekana." alifunguka Nahreel kwenye 255 ya XXL Clouds FM, na kuendelea,
-
"We are proud kwa kutengeneza kitu au kutengeneza wasanii ambao leo hii wanajulikana. Kwa hiyo kusaini dili nyingine ni kitu kizuri na kikubwa sana, na ndio maana na sisi tulifungua record label kwa lengo la kusapoti. Hivyo Rosa Ree anapopata sapoti nyingine na mimi naendelea kuwa na roho ile ile ya kusapoti. Naamini itamfikisha sehemu ambayo mimi pengine nisingeweza." - alimaliza Nahreel.

Baada ya kuondoka The Industry, Rosa Ree alifanya mikwaju kama: Dow na Marathon and now anatamba na dude lake jipya, WAY UP ft. Emtee ambayo ni ngoma ya kwanza chini ya Uongozi wake mpya DIMO PRODUCTION

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad