Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule (Proffesor Jay) jana alisema kuwa zaidi wananchi 40 wa kata ya Luhembe, Jimbo la Mikumi wamepotea na hawapatikani.
Mbunge huyo alihoji Serikali ina sema nini juu ya wananchi hao wanaopotea na hawaonekani na tabia ya watumishi wa TANAPA kuwachukua wakazi wa Mikumi na kuwatesa.?
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga alimuagiza ‘Prof. Jay’, kupeleka ushahidi wa madai yake ili serikali iyafanyie kazi.
Hasunga alisema; "Mheshimiwa Mbunge naomba ulete ushahidi wa kupotea kwa wananchi ili kutanabaisha taarifa hizo na serikali itashughulikia suala hilo maana serikali ipo kwa kulinda usalama wa wananchi”.
Naibu Waziri aliongeza kuwa serikali tayari imetatua mgogoro wa mpaka kati ya wakazi wa Mikumi na maeneo ya hifadhi.