Rais Magufuli Afurahishwa na Swali Aliloulizwa na Mwananchi...Kampa Laki 2 na Kuahidi Barabara Itayojengwa Ipewe Jina Lake


Rais John Magufuli ametaka barabara itakayokarabatiwa karibu na eneo la Msikiti Mkuu wa Bakwata Kinondoni ipewe jina la mkazi aliyejitambulisha kwa jina la Rashidi Masushi baada ya kusema swali lake lina  maslahi kwa wananchi wa eneo hilo.


Masushi alipewa fursa ya kuuliza swali wakati Rais Magufuli alipowasalimia kwa muda wakazi eneo hilo leo Juni 12, baada ya kumaliza ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Bakwata Kinondoni.


Mkazi huyo alimwomba Rais Magufuli asaidie kufanikisha ukarabati wa eneo lililopo karibu na msikiti huo akidai limekuwa likiwapa wakati mgumu wananchi wake kutokana na kujaa maji mara kwa mara.


“Mheshimiwa rais hapo karibu na msikiti kuna dimbwi la maji ambalo linatufanya wakati mwingine tuwe katika wakati mgumu tunapokwenda msikitini. Kwa vile wakati fulani wewe ulikuwa mkazi wa eneo hili la Kinondoni na mimi ni mjumbe wa nyumba kumi naomba tufanyie mipango ili angalau nasi tuondokane na adha hii,” alisema.


Baada ya maelezo hayo Rais Magufuli alianza kwa kusema: “Swali nzuri sana na nadhani ameuliza kwa niaba ya wananchi napenda wananchi wa namna hii ... hebu tumpigie makofi Rashid.  Mkuu wa mkoa ebu chukua namba yake ili barabara hii ianze kukarabatiwa mara moja na kazi hii ifanyike kwa fedha za mfuko wa barabara....naagiza kazi ifanyike mara moja,” aliagiza Rais Magufuli.


Wakati mkuu wa mkoa, Paul Makonda akibadilishana namba na Masushi, Rais Magufuli alimwita tena mkazi huyo na kumuuliza: “ Hivi bwana Rashid unafanya kazi gani?”


Masushi amejibu:  “Nina kibanda changu cha biashara,” alijibu na kumfanya Rais Magufuli atabasamu.


Magufuli akasema:  “ Njoo uchukue laki moja hapa ukaongezea biashara yako.” Alikwenda na kukabidhiwa Sh200,000.


“Haya uende ukaongezee kwenye biashara yako na kuanzia sasa barabara hii itakapotengenezwa itaitwa Rashid Masushi,” amesema Rais Magufuli.


Baada ya kupokea fedha hizo alirejea tena sehemu alikokuwa amesimama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na kisha akatoa noti ya Sh10,000  na kumpa tukio ambalo lilimfanya Makonda aungue kicheko huku akirejea sehemu alikosimama awa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad