Rais Magufuli Awataka Mabalozi Wake Kutafuta Masoko

Rais Magufuli Awataka Mabalozi Wake Kutafuta Masoko
Rais John Pombe Magufuli amewataka mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kuhakikisha wanatafuta masoko ya mazao ya kilimo katika nchi wanazoziwakilisha.


Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akizindua Program ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

"Moja ya jukumu kubwa la mabalozi wetu huko waliko ni kutafuta fursa zitazoisaidia Tanzania kukua kiuchumi, na hili la kutafuta masoko ya mazao pia linawahusu." Magufuli.

Katika uzinduzi huo Rais Magufuli amewaonya wale wanaorudisha nyuma sekta ya kilimo na kuwataka viongozi wenye dhamana ya kuhakikisha kilimo kinawakomboa wananchi wawe wabunifu katika kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo, uvuvi na ufugaji.

Aidha amesema, ukosefu wa masoko wa bidhaa zinazozalishwa nchini, unarudisha nyuma maendeleo na kueleza kushangazwa kwake na uwepo wa tozo nyingi zinazosababishwa na Bodi ambazo hazina msaada wa moja kwa moja kwa wakulima.

Pamoja na hayo Rais Magufuli amewashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo wabia wa maendeleo wa kimataifa kwa kufanikisha mradi huo, na kusisitiza kuwa iwapo kila mdau atasimamia jukumu lake kwa uadilifu na kujituma, Tanzania ya Uchumi wa kati ifikapo 2025 litafanikiwa.

Programu hii iliyozinduliwa leo ni ya miaka mitano na itagharimu shilingi trilioni 13.8.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad