Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuzuru nchini Kenya mwezi ujao katika ziara ambayo itakuwa ya kihistoria.
Uhuru Kenyatta na Rais Magufuli kwenye picha alipofanya ziara ya kwanza nchini Kenya mwaka 2016
Rais Magufuli kwenye ziara yake ataungana na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga na kisha kutembelea katika Kaunti ya Nyanza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la Nation la nchini Kenya limeeleza kuwa Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili nchini Kenya Ijumaa ya wiki lijalo.
Gazeti hilo pia halijaeleza ziara hiyo itakuwa ya siku ngapi na itakuwa na lengo gani katika kipindi hiki ambacho Rais Uhuru Kenyatta na Odinga wameonekana kupatana na kuweka tofauti zao za kisiasa kando.
Hii ni mara ya pili kwa Rais Magufuli kuzuru nchini Kenya ni baada ya kuzuru mwaka jana ambapo alikutana na Rais Uhuru Kenyatta.
Hata hivyo, Rais Magufuli hata kabla ya kukutana na Kenyatta mwaka 2016 kwenye ziara yake nchini Kenya mwaka huo huo alitembelewa na Raila Odinga kijijini kwake Chato..
Ziara hiyo inakuwa ni ya kihistoria na ya kwanza kwa Rais Magufuli kukutana na viongozi hao wawili na wenye nguvu zaidi kwenye siasa za Kenya.