Rais Museveni Atajwa kuwa Miongoni Mwa Marais Bora Kote Ulimwenguni

- Rais wa Uganda Yoweri Museveni alitajwa kuwa miongoni mwa marais bora kote ulimwenguni
- Museveni anasemekana kuchangia asilimia 2.42% ya kukuza maendeleo na uchumi wa nchi yake tangu alipoingia mamlakani mwaka wa 1986
- Aliwashinda viongozi shupavu akiwemo aliyekuwa waziri mkuu wa Singapore, Lee Kuan Yew Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ametajwa kuwa miongoni mwa marais bora zaidi kote ulimwenguni.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 74 na ambaye amekuwa mamlakani kwa zaidi ya miaka 30 alipewa nambari 12 kwenye orodha ya viongozi 24 ulimwengu mzima ambao wamechangia pakubwa katika kukuza uchumi katika mataifa yao. 

Kulingana na takwimu za profesa mmoja wa masuala ya kiuchumi kutoka chuo kikuu cha New York na pia mchumi wa Benki ya Dunia Steven Pennings, Museveni alichangia asilimi 2.42% katika kuendeleza uchumi wa Uganda tangu alipoingia mamlakani.

Udaku iliweza kubaini kuwa, marais wawili pekee kutoka Afrika; Museveni na aliyekuwa rais wa Botswana Seretse Ian Khama ndio waliotajwa kuwa bora kulingana na ripoti ya Pennings. 

Khama alistaafu katika siasa baada ya kutawala Botswana kwa miaka 10 kutoka mwaka wa 2008 hadi 2018. 

Kwa ujumla rais wa Burma, Than Shwe ambaye aliitawala nchi hiyo kutoka mwaka wa 1992 hadi 2011 ndiye aliyetajwa kuwa rais bora zaidi kote ulimwenguni. Wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ya Pennings ni rais wa Ecuado, Guillermo Rodriguez Lara na aliyekuwa waziri wa Malaysia, Najib Razak. 
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad