Kiongozi wa Korea Kaskazini KIM JONG UN amesema kuwa mpango wake wa kusitisha majaribio ya nyuklia utakua wa hatua kwa hatua kinyume na matakwa ya Marekani.
Awali Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo alisema kuna maendeleo makubwa kutokana na mazungumzo dhidi ya maafisa wa juu wa Korea Kaskazini lakini alikataa kuhakikisha mazungumzao kati ya Trump na Kim Jong.
Pompeo Ameongeza pia kuwa ikiwa mazungumzo baina ya viongozi hao wawili yataenda sawa basi litakuwa ni jambo la Kihistioria na lenye kuleta Maendeleo ya dunia.
Pompeo na afisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini, Kim Yong Chol wanaendelea na mazungumzo yao mjini New York, kujaribu kuandaa mkutano wa kilele kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong Un akiwa ni afisa wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini kuizuru Marekani katika kipindi cha miaka 18.