Rais wa Syria, Bashar al-Assad anapanga kutembelea nchini Korea Kaskazini,Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeeleza.
Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuhodhi ziara ya Kiongozi wa nchi tangu alipoingia marakani mwaka 2011
Hivi karibuni amekuwa na shughuli nyingi za kidiplomasia, kukutana na Rais wa China mwezi Mei na anatarajiwa kuhudhuria mkutano na Donald Trump mwezi huu
Syria, mshirika wa Korea Kaskazini, haijasema lolote kuhusu mpango huo unaoripotiwa.
Nchi hizi mbili zimekuwa zikishutumiwa kushirikiana katika mapngo wa kutumia silaha za kemikali.Lakini nchi hizi zimekana shutuma hizo
Tarehe ya ziara hiyo haijawekwa wazina vyombo vya Korea Kaskazini.
Vilimnukuu bwana Assad siku ya Jumatano akisema ''ninakwenda kutembelea Korea Kaskazini na kukutana na Kim Jong-un."
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili ulianza mwaka 1966 na kutuma vikosi na silaha wakati wa vita vya Arab na Israeli mwezi Oktoba mwaka 1973
Ripoti ya Umoja wa mataifa ilivuja mwezi Februari ikishutumu Korea Kaskazini kwa kufanya safari za meli takriban 40 kuelekea Syria kati ya mwaka 2012 na 2017, meli zinazodaiwa kubeba acid, mipira na bidhaa nyingine zinazodaiwa kuw zinaweza kutengeneza silaha za kemikali.
Assad ameshutumiwa kutumia silaha za kemikali wakati wa vita vya miaka saba nchini humo lakini amekana kuwa na kemikali hizo.
Credit: BBC