Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa amewashangaza watu baada ya kuonekana kwa mama ntilie akiwa amepanga foleni kwa ajili ya kununua kuku wa kukaanga.
Tukio hilo la aina yake lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Rais huyo alipigwa picha akiwa amepanga foleni akiwa na wananchi wa kawaida huku akiwa anasubiri kupatiwa huduma ya kuku wa kukaangwa.
Kitendo hicho kimetajwa kwamba ni mwonekano tofauti na utawala uliopita kwani Rais huyo anapenda kujichanganya na wananchi wa kawaida kuliko mtangulizi wake, Robert Mugabe.
Rais Mnangagwa alionekana akiwa amepanga foleni hiyo kwenye kibanda cha mama ntilie mmoja kilichopo katika mji mdogo wa Chegutu uliopo kilomita 100 kutoka mji mkuu wa Harare.
“Baada ya foleni yake kufikiwa aliagiza vipande viwili pamoja na Juisi vyenye gharama ya Dola 3.75 kisha akatoa Dola 20 na kuniambia nisimrudishie chenji inayobaki, alisema Isabel Mtongerwa aliyekuwa akimhudumia Rais Mnangagwa.
Mwanasiasa huyo anakuwa karibu zaidi na watu kutokana na kutumia sana mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter ukilinganisha na mtangulizi wake.