Rais wa Zimbabwe Atembelea Bagamoyo.... Amwaga Dola Elfu 10

Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Emmerson Mnangwaga leo asubuhi ametembelea iliyokuwa shule ya wapigania uhuru wa chama cha FRELIMO ambacho hivi sasa ni Chuo cha Kilimo na Mifugo cha Kaole kilichopo Bagamoyo Mkoani Pwani.



Rais Mnangwaga akiwa chuoni hapo amesema yeye ni mojawapo ya waanzilishi wa chuo hicho katika miaka ya sitini akiwa pamoja na viongozi wengine wa Chama cha FRELIMO na kwamba alikuwa kiongozi wa ulinzi wa chuo hicho na kwamba hawakuwa na dhumuni la kutafuta madaraka bali ilikuwa ni jitihada zilizosukumwa na uzalendo wa kuzipatia nchi zao uhuru,” Rais Emmerson Mnangwaga.

Rais Mnangwaga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa kumpa fursa ya kuitembelea Shule hiyo kwa kuwa ilikuwa ni shauku yake baada ya kuondoka shuleni hapo miaka 58 iliyopita na kuwashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kumtunza katika kipindi chote alichoishi Bagamoyo na kwamba hata sasa anajisikia kuwa ni mmojawapo wa jamii ya watu wa Bagamoyo,” Amesema Rais Mnangwaga.

Pia Rais Mnangwaga ametoa kiasi cha Dola elfu kumi kwa mkuu wa chuo hicho kama shukrani yake ambazo amesema zitasaidia kutatua baadhi ya changamoto chuoni hapo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad