Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Awasili Dar Kukuza Uhusiano

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Awasili Dar Kukuza Uhusiano
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amewasili Dares salaam katika ziara ya kwanza nchini humo tangu aingie madarakani.

Ni ziara ya siku mbili ambayo imetajwa kulenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje.

Amewasili asubuhi hii na kupokewa na mwenyeji wake Ras John Pombe Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akiwa Tanzania kiongozi huyo anatarajiwa kutembelea chuo cha kilimo alikosomea miongoni mwa wapiganjiaji uhuru waliotoka nchi za kusini mwa Afrika.

Itakumbukwa kwamba Rais Magufuli alikuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika waliompongeza rais Mnangagwa kwa kuchukua uongozi wa nchi pasi kushuhudia ghasia za aina yoyote.

Huenda ziara hii inafuata mualiko rasmi kwa Mnangagwa kutoka rais Magufuli uliowasilishwa na ujumbe wa chama tawala CCM ulioongozwa na aliyekuwa katibu mkuu Abdulrahman Kinana waliokwenda Zimbabwe mwezi uliopita.


Kinana alifanya ziara hii mwishoni mwa mwezi may kabla ya kuachia ngazi kama katibu mkuu wa CCM.

Mnangagwa, aliingia madarakani mnamo Novemba kufuatia mapinduzi ya jeshi dhidi ya kiongozi mkongwe Robert Mugabe.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad