Rapa Offset Amethibitisha kuwa The Best Hip Hop Female Artist kwa sasa Card B ni Mke wake


Rapa Offset Amethibitisha kuwa The Best Hip Hop Female Artist kwa sasa @iamcardb ni Mke wake, kupitia maneno aliyoyaongea kwenye usiku wa tuzo za Bet zilizofanyika huko Los Angels Marekani Jumapili hii.

Licha ya Maneno ya @offsetyrn , lakini pia Mwanadada huyo anayetarajia kupata mtoto hivi karibuni, alidondosha ujumbe mzito kwenye ukurasa wake wa Twitter ukionesha kuwa hajapata mtoto nje ya ndoa.

Kupitia Mtandao wa TMZ wa Marekani, Cheti walichokiweka katika page zao kinaonesha kuwa wawili hao walifunga ndoa kwa siri tangu tarehe 20 Septemba 2017.

Ukifuatilia Clip mbalimbali Utagundua kuwa wawili hawa walivalishana Pete ya Uchumba hadharani kitambo lakini swala la ndoa hawakulitangaza na kulifanya kama siri.

Card B alivalishwa pete ya Uchumba Miezi 10 Iliyopita na wiki chache baadae akatangaza kuwa ni Mjamzito, kitu kilichonukuliwa kama alifanya hivyo baada ya kuwa Confirmed sasa ni Mke Halali wa Rapa @offsetyrn

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad