RC Ashtakiwa na Wanakijiji kwa Magufuli



Wanakijiji  wa kijiji cha Remng'orori wilayani Serengeti wamemshtaki Mkuu wa mkoa wa Mara,  Adam Malima kwa Rais John Magufuli kwamba anataka kuwapora ardhi yao wanayotegemea kwa kilimo na kuwapatia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili waweke kambi yao.

Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, wameiambia Nipashe kuwa amri ya Malima imewasababishia ugumu wa maisha kwa kuwa mwaka huu hawakulima katika ardhi hiyo ambayo ipo mpakani mwa wilaya za Serengeti na Butiama mkoani Mara.

Mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Motiba Maro akizungumza na Nipashe amesema, wananchi wa kijiji hicho wameshindwa cha kufanya kilimo kutokana na amri hiyo ya Malima na kumuomba Rais Magufuli kuingilia kati.

"Hapa huu mgogoro umemshinda Malima, lazima Rais atume wasaidizi wake waje wasikilize malalamiko yetu, ili tupate haki yetu," amesema.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa kijiji cha Remng'orori, Msamba Maro amekiri wananchi wake kuzuiwa kulima katika eneo hilo, hatua ambayo imewaathiri kwa kuwa mwaka huu watakabiliwa na baa la njaa.

Msamba amesema eneo hilo lina mgogoro unaohusisha vijiji viwili vya Remng'orori na Mikomariro na mwanzoni mwa mwaka huu ulisababisha mapigano yaliyosababisha vifo vya watu wawili waliouawa mwanzoni mwa mwaka huu ulisababisha mapigano yaliyosababisha vifo vya watu wawili waliouawa kwa kukatwa mapanga.

Mapema mwaka huu Malima akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, alikiri kwamba mgogoro huo unasabababishwa na wavamizi kutoka nchi jirani ya Kenya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad