RC Makonda Noma...Apigania Hati ya Nyumba ya Bi Zainab Mpaka Imepatikana..Tazama Video

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amekabidhi hati ya nyumba ya Bi Zainab na mumewe ambayo ilikuwa mikononi mwa Benki ya FNB kutokana na mgogoro wa eneo lao kuwa na deni katika benki hiyo.

 Bi Zainab alipata umaarufu mkubwa kufuatia sakata lake la kununua eneo ambalo hakuwa na taarifa nalo na kujenga nyumba bila kufahamu kuwa aliyemuuzia eneo hilo alikuwa amekopa benki kwa kuweka rehani eneo hilo.

 Siku chache baada ya kujenga watu wa Benki walifika na kuanza taratibu za kuuza nyumba yake, lakini sakata hili lilitua mikononi mwa RC Makonda ambaye alichukua hatua za awali kwa kustopisha zoezi la kuuza nyumba hiyo.

 RC Makonda amekabidhi hati hiyo kwa Shabani Amiri ambaye alifika kwa ajili ya kumuwakilisha Bi Zainab ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akimuuguza Mumewe anayesumbuliwa na tatizo la moyo lililotokana na mshtuko baada ya Benki hiyo kutaka kuuza nyumba yao.

VIDEO:

Source:GPL
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad