Tume ya uchaguzi nchini Uturuki imemtangaza Rais Recep Tayyip Erdogan kama mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika June 24.
Erdogan ambaye aliingia madarakani 2014 ameshinda muhula wake wa pili kwa ailimia 53 ya kura zote zilizohesabiwa akiepuka kuingia mzunguko wa pili huku chama chake kikishinda wingi wa viti bungeni.
Mpinzani wake mkuu Muharrem Ince kutoka chama cha CHP tayari amempongeza Erdogan katika mitandao ya kijamii licha ya kushutumu uchaguzi huo kuwa haukuwa wa haki.
Muda mfupi kabla ya kura halisi kutangazwa Erdogan alizungumza kupitia televishen ya taifa akisema taifa lake limepata taarifa nzuri za yeye kuendelea kusalia madarakani licha ya kwamba hazikua bado za uhakika.
''Uchaguzi wa June 24 umeleta taarifa nzuri kwa nchi yetu, kwa watu wetu. Kwa taarifa nilizonazo licha ya kuwa sio za uhakika ni kwamba nchi yetu imenichagua kuendela kuwa rais, licha ya kuwa sio za uhakika. Pia chama cha AK kimeshinda uwakilishi wa viti vingi bungeni, ambapo tuna shughuli za kisheria.'' Alisema Erdogan.