Sakata la Trillion 1.5, Serikali yafunguka Zilipo Billion 204 Sehemu ya Hela Hizo


SAKATA LA TRILIONI 1.5, Serikali yafunguka kuhusu Tsh. Bilioni 204 ambazo ni sehemu ya sakata la Tsh. Trilioni 1.5 zinazodaiwa kutopelekwa Zanzibar na kusema kuwa ziliingizwa moja kwa moja kwenye akaunti ya Mlipaji Mkuu wa Serikali ya Zanzibar

Kwa mujibu wa Mhe. Zitto Kabwe(ACT-Wazalendo), Ufafanuzi huo ulitolewa Bungeni jana Juni 08, na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Konde(CUF), Khatib Said Haji

Mbunge Konde alihoji kuwa Serikali wakati ikitoa ufafanuzi kuhusu suala la kutoonekana Tsh. Trilioni 1.5, ilieleza kwamba kati ya fedha hizo Tsh. Bilioni 204 ni makusanyo ya Zanzibar. “Sasa Waziri kabla hazijatumbukia kuwa kwenye kero ya Muungano ni lini fedha hizi zitafika Zanzibar?”

Dkt. Kijaji alipokuwa anajibu alisema “Fedha hizi hukusanywa na TRA inayofanya kazi Zanzibar na zinapokusanywa fedha hizo zinasomeka kwenye taarifa za fedha TRA kwasababu zinakusanywa na TRA,”

Aidha, Dkt. Kijaji aliongeza kuwa fedha hizo hazivuki maji kuja Tanzania bara bali zinaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya mlipaji mkuu wa serikali ya Zanzibar

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad