DAR: Serikali imesema inafuatilia sakata la walemavu kutoka nchini waliopelekwa Kenya kufanya biashara ya kuwa ombaomba
Katika sakata hilo, hivi karibuni vyombo vya habari nchini Kenya vilitangaza taarifa ya kukamatwa kwa watu watano ambao wanahusishwa na kusafirisha walemavu hao
Katika habari hizo na kupitia mitandao ya kijamii kulisambaa video ndogo iliyoonesha Watanzania wawili, waliotambulika kwa majina ya Moshi na Jasa Mila wakiwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa na Polisi
Akizungumzia tukio hilo jana, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk Anna Makakala alisema taarifa hizo ameziona kupitia mitandao ya jamii na kwamba, ufuatiliaji umeanza kufanywa na idara yake
Inadaiwa watu hapo wanaowapeleka walemavu Kenya huingia makubaliano na wazazi wa walemavu(Kwa walemavu wenye wazazi) ya kuwalipa Tsh. 150,000kwa mwezi, muda mwingine makubaliano ni ya kugawana kinachopatikana kutoka kwa mlemavu baada ya kuombaomba