Sakaya Amkingia Kifua Maalim Seif bungeni
0
June 06, 2018
NA FATUMA MUNA
Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya ameweka wazai kuwa yeye ndiye anayepaswa kuhojiwa kuhusu matumizi ya Chama cha Wananchi (CUF) na si Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.
Sakaya ametoa kauli hiyo leo bungeni Juni 5, 2018 wakati akichangia hoja ya Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji aliyetaka Maalim Seif kuhojiwa kwa kutokupeleka taarifa za CUF kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
“Maalim Seif toka mwaka 2016 hayuko ofisini. Mimi ndiye najua matumizi ya CUF napaswa kuhojiwa. Suala la kusema Serikali imetoa fedha, ruzuku imetolewa kwa CUF kama taasisi na Takukuru ije kunihoji mimi na si Maalim Seif. "Huwezi kujua mambo ya ofisi kama hauko ofisini, hawezi kujua mambo ya ofisini kama yuko mitaani,” amesema.
Awali Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kutokupeleka taarifa za matumizi za chama kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Akichangia bajeti ya wizara ya fedha na mipango ya mwaka 2018/19 leo bungeni Juni 5, 2018, Khatibu alisema kwamba Seif hajakitendea haki Chama kwa kuacha kupeleka hesebu kwa CAG.
“Kama chama changu kimeshindwa kupeleka taarifa zake kwa CAG kukaguliwa na kama hakijapeleka, Napata wapi ujasiri wa kuhoji Sh1.5 trilioni?.
Tags