Samatta Awaaga Wawakilishi Tanzania Kwenye Michuano ya Golf

Samatta awaaga wawakilishi Tanzania
Nyota wa soka wa Kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, mapema leo asubuhi amekutana na kuwaaga Mabingwa wa mnchezo wa Golf  nchini ambao wanasafiri kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Golf Africa.


Mabingwa hao ambao ni Angel Eaton kwa upande wa wanawake na Victor Mwene kwa upande wa wanaume wameondoka leo asubuhi kuelekea nchini Namibia ambako watakuwa wanawania ubingwa wa Africa wa Golf.

Mashindano hayo maarufu kama (Windhoek Lager Africa Jacket Championship), yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Juni na yatafanyika kwenye Mji mkuu wa Namibia Windhoek katika viwanja vya Windhoek Golf na Country Club.

Samatta amewaomba Watanzania kuungana kwa pamoja na kuwatakia kila la kheri wawakilishi hao ili waweze kuibuka na ushindi na kuleta heshima nchini pamoja na wao kujitangaza kimataifa zaidi.

''Bahati ilioje nimekutana na mabingwa wa Golf  Tanzania ambao wanasafiri kwenda kwenye mashindano ya Golf Africa huko Namibia tuwatakie kila la kheri katika mashindano watuwakilishe vyema watanzania'', ameandika Samatta.

Tags

Top Post Ad

Below Post Ad