Sanaa Hailipi Tena Umachinga ndo Unaniokoa- Mwanaheri

Sanaa Hailipi Tena Umachinga ndo Unaniokoa- Mwanaheri
MUIGIZAJI wa Bongo Muvi, Mwanaheri Ahmed amefunguka kuwa umachinga anaoufanya nje ya uigizaji umemsaidia kwa sababu isingekuwa hivyo maisha yangekuwa ni magumu kwani sanaa hailipi tena kama ilivyokuwa awali.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Mwanaheri ambaye kwa hivi sasa amefungua duka lake la kuuza madera Tandika jijini Dar, alisema amefanikiwa hilo baada ya kuuza nguo mojamoja mtaani mpaka kufikia hatua ya kufungua duka lake mwenyewe baada ya kuweka aibu pembeni.

“Mimi ningejifanya naona haya basi nisingefikia lengo hata kidogo lakini kwa sababu niliweka mambo ya ustaa pembeni nikachagua kufanya maisha ndio maana mpaka sasa hivi Mungu kanibariki siwezi kusema nitakosa hata hela ya kula, ningesubiria filamu zangu ziuze basi ningekuwa kwenye wakati mgumu sana,” alisema Mwanaheri.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad