"Serikali Imewapa Watanzania Ugali,Tembele" Mtolea

"Serikali imewapa Watanzania ugali,tembele" Mtolea
Mbunge wa Temeke, (CUF) Abdallah Mtolea, amesema kwamba serikali inajua kwamba inawadhihaki watanzania kwa kudai kuwa uchumi unakuwa huku kiuhalisia wanafahamu fika hakuna kilichoongezeka ndiyo maana majukwaani hawazungumzii suala la mlo bora kwa watanzania bali wanakuwa wanazungumzia sifa

Mh. Mtolea ameyasema hayo wakati akichangia hoja katika mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya serikali 2018 / 2019 iliyowasilishwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango.

Amesema kabla ya Waziri kuwasilisha Bajeti alizungumzia hali ya uhumi nchi kwamba inazidi kukua lakini kiuhalisia alichokiona yeye kilichoandikwa kina lengo la kuwafurahisha wazungu au Benki ya Dunia ili kuonyesha kuwa serikali ya Tanzania bado ina sifa ya kuweza kukopa.

Mtolea amesema kwamba kitendo cha serikali kudaii kuwa wamewezesha pato la kila mtanzania kuongezeka ni kejeli kwani hicho kiasi kilichoongezeka ni kiasi ambacho hakimpatii mtanzania milo mitatu zaidi ya kwamba itamptia ugali na tembele la kuchemsha.

"Serikali ya CCM inapenda sifa sana ndiyo maana majukwaani utasikia inasema kwamba wamenunua ndege, sijui miradi ya  Stigler's Gorge,, Standard Gauge lakini husikii wakisifia kuwa tumewezesha kula ugali na tembele la kuchemsha kwa sababu wanajua kuwa siyo sifa bali ni kejeli kubwa kwa watanzania" Mtolea.

Hata hivyo Mtolea ameongeza kwamba hata kitendo cha serikali kusema umri wa kuishi wa watanzania umeongezeka ni kejeli na kwamba mu kufikisha miaka 64 ni kawaida  na siyo ajabu kwa watu wenye maisha duni kutimiza umri huo endapo wataakuwa hawapati magonjwa.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad