Serikali Yaamua Kuongeza Likizo ya Uzazi kwa Akinamama

Serikali inaandaa utaratibu utakuowezesha kuongeza muda wa likizo ya uzazi kwa akinamama waajiriwa ambao watajifungua watoto kabla ya wakati, ili kusaidia kutenga muda wa kutosha kwa wazazi kuwa karibu zaidi na watoto hao.


Hayo yamesemwa leo Juni 11, 2018 Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu, Mh. Jenista Mhagama, amesema kuwa Serikali imepokea maombi megi kuhusu jambo hilo na kuongeza kwamba likizo hiyo haitawanufaisha akinamama pekee bali bali hata wazazi wakiume wa watoto hao.

“Naomba nilihakikishie Bunge lako tukufu kuwa, hayo ni mambo ambayo yanaendelea kujadiliwa na kufanyiwa kazi ili kuweza kuwasaidia wanawake lakini hata wanaume ambao wake zao wamejifugua watoto ambao wamezaliwa kabla ya umri wao, ili waweze kupewa haki na kusaidia malezi ya watoto na malezi ya familia kwa ujumla” amesema Waziri Mhagama.

Waziri Mhagama ameongeza kuwa Serikali itaendelea kubadili baadhi ya sheria za afya ya uzazi hasa kwa akina mamna wanaopata changamoto mbalimbali wakati wa kujifungua ili kuweza kuwasaidia wafanyakazi nchini.

Sheria ya Ajira na Mahusiano ya kazi ya mwaka 2004, inampa mama mjamzito ambaye ni muajiriwa likizo ya miezi mitatu kabla ya kujifungua, na atatakiwa kurudi kazini wiki sita baada ya kujifungua, pia sheria hiyo inatoa likizo ya siku tatu kwa baba wa mtoto baada ya mama kujifungua.
Chanzo EATV
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad