Serikali Yaikana Barua Ilioiandikia Kanisa la KKT Ikiiitaka Kufuta Waraka wa Pasaka

Serikali Yaikana Barua Ilioiandikia Kanisa la KKT Ikiiitaka Kufuta  Waraka wa Pasaka
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Waraka wa barua unaodaiwa kuandikwa na Serikali dhidi ya Makanisa unaosambaa mitandaoni si wa kweli na kwamba ni uhalifu umefanywa na watu wasioitakia nchi mema.

Waziri Nchemba amesema Serikali haipingani na dhehebu lolote na pale ambapo kuna uhitaji wa kufanyia kazi jambo kuhusu taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo taratibu huwa zinatumika kuzungumza na sio kama ilivyofanywa taarifa hiyo inayosambaa.

Serikali inalinda uhuru wa kuabudu na waumini hivyo taarifa hiyo inayosambaa ni batili na tayari uchunguzi umeanza kufanyika.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo

Dk Nchemba amesema amefuatilia barua hizo na kuona zina mkanganyiko wa anuani.

Viongozi wa dini wasiwe na taharuki na taarifa hizo, hazina baraka za Serikali. Wasisite kuwasiliana na Serikali kujua uhalali wake.

Dk Nchemba amesema waraka wa viongozi wa dini uliotolewa miezi iliyopita ni jambo lililopita na hivyo akawataka viongozi wa dini waendelee na kazi zao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad