Serikali yaondoa vibali wanaosafirisha samaki wa kitoweo


Serikali imeondoa sharti la wananchi wanaosafirisha samaki kwa ajili ya kitoweo kuwa na vibali.


Uamuzi huo uliotangazwa jana Juni 24, 2018 mjini Sengerema na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina utahusisha wananchi wanaosafirisha samaki wa kitoweo hadi kilo 20 kutoka sehemu moja kwenye nyingine.


Akizungumza wakati wa uteketezaji wa zana haramu za uvuvi zenye thamani ya zaidi ya Sh2.3bilioni, kati yake zikiwemo zana zenye thamani ya Sh1.5 bilioni za mfanyabiashara Josefu Kando (Njiwa Pori), Waziri Mpina amesema uamuzi huo wa Serikali unalenga kutoa fursa kwa wananchi kufaidi na kutumia rasimali za Ziwa Victoria.


Pamoja na kufuta vibali vya kusafirisha kitoweo, Waziri Mpina amesisitiza kuendelea kwa operesheni dhidi ya uvuvi haramu huku akiwaagiza wanaoendelea kumiliki zana haramu za uvuvi kuzisalimisha kabla hawajafikiwa ya mikono mirefu ya dola.


Mkuu wa opereshemi dhidi ya uvuvi haramu wilayani Sengerema, Wenceslaus Luhasile ameahidi kuendeleza vita dhidi ya uvuvi haramu na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano wanapobaini vitendo hivyo katika maeneo yao na kuahidi kutunza siri za wanaotoa taarifa.


Kauli hiyo iliungwa mkono na mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole aliyeongeza kuwa jukumu la kulinda rasilimali za nchi ni la kila Mtanzania kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad