Serikali kupitia Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 imepanga kutumia shilingi 22.5 kwaajili ya matumizi ya uzazi wa mpango.
Akizungumza leo, Juni 13, 2018 Bungeni Jijini Dodoma, Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu amesema kutoka katika vyanzo vya ndani kiwango hiki ni sawa na ongezeko la asilimia 60 kutoka mwaka 2017/2018.
“Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi Bilioni 22.5 kwaajili ya uzazi wa mpango kutoka katika vyanzo vya ndani kiwango hiki ni cha fedha sawa na ongezeko la asilimia 60 kutoka mwaka 2017/2018,” amesema Ummy.
Hayo yameelezwa baada ya Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi kuihoji serikali kuwa “Mahitaji halisi ya fedha kwaajili ya uzazi wa mpango kwa mwaka kwasasa ni zaidi ya Sh. Bilioni 36 , Je, Serikali ina mpango gani wa kutenga fedha zaidi ili kufikia kiasi kinachohitajika kwaajili ya wakina mama na watoto?”