Serikili yanuia kufungua fursa za kibiashara katika Kimondo cha songwe


Wawekezaji na wafanyabiashara wametakiwa kujikita kwenye uwekezaji wa kimondo kilichopo mkoani songwe eneo ambalo linafanyiwa marekebisho hivi sasa ambapo itaandaliwa  hafla kubwa  itakayofanyika siku ya maadhimisho ya kimondo duniani ambayo hufanyika kila mwaka juni 30, ikiambatana  na ugawaji wa maeneo ya uwekezaji wa miradi mikubwa ikiwemo hotel, viwanja vya kisasa vya michezo, kumbi za starehe, pamoja na fursa mbalimbali za uchumi.

Muungwana blog imetembelea kimondo hicho na kuzungumza na baadhi ya watalii waliofika eneo hilo ambao  mbali ya kuona kama ni nafasi ya kipekee kukiona kimondo hicho pia wameahidi kuwa mabalozi huko wanakokwenda, lakini wametaja dosari ya miundombinu ya mradi huo.

Zainabu Vullu ni mmoja wa watalii waliofika eneo la kimondo amesem kuwa licha ya kuwa ni mara yake ya kwanza kufika kujionea kivutio hicho lakini ameomba watanzania kujifunza kuthamini wao kwanza kuliko wageni wanakuja kufaidi kuona na kujua historia ya kimondo huku wenyeji wakishindwa kutumia fursa hiyo huku Jasmine Tisekwa akisema kuwa kuanzia sasa baada ya kufika eneo la kimondo cha mbozi watakuwa mabalozi wazuri kwa watanzania wengine.

Mkuu wa mkoa wa songwe bi. CHIKU GALLAWA amesema ni wakati mwafaka sasa  wawekezaji kujitokeza na kuwahi nafasi za kuwekeza kwenye eneo la kimondo kwa kuwa maboresho ya sasa yataibua fursa mbalimbali za kiuchumi na biashara na kuongeza  mahitaji ya huduma za jamii.

 Aidha  mkuu wa mkoa amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa wa songwe  kuhakikisha wanaungana  na kufanya maboresho ya miundombinu ya eneo la kimondo kilichopo katika kijiji cha ndolezi kata ya mlangali wilayani mbozi lengo ni kupanua fursa za uwekezaji kupitia kimondo hicho
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad