Shaffih Dauda in Russia na Unayotakiwa Kufahamu Kuelekea Kombe la Dunia

Jana asubuhi baada ya kutoka kwenye mwaliko wa ubalozi wa Tanzania nchini Urusi niliondoka na kuelekea kwenye mji wa St. Petersburg na kwa mara ya kwanza niliweza ku-experience matumizi ya Fan ID. Nilitumia Fan ID yangu kusafiri kwa train kufika St. Petersburg kujionea maandalizi yapoje na kitu gani kingine kipo hapa.

Mwenzangu Edgar Kibwana nilimwacha Moscow, Aziz Kindamba alielekea katika mji wa Kazan Benny On-air yeye akaenda Kaliningrad. Wote kwa pamoja tunajaribu kutembea katika miji tofauti kuweza kufahamu nini kinaendelea na kukupatia msomaji wetu taarifa za moto moto kutoka hapa Urusi.

Ikumbukwe miji 11 ita-host michuano ya fainali za kombe la dunia hapa Urusi hadi kufika mwisho July 15, 2018 siku ambayo tugashuhudia mchezo wa fainali katika uwanja wa Luzhniki katika jiji la Moscow.

WAANDISHI WA HABARI

Baada ya kufika St. Petersburg mji ambao ni wa pili kwa ukubwa ukitoa jiji la Moscow, nikataka kujua mimi kama mwandishi wa habari nimeandaliwa mazingira gani ya kufanya kazi bila usumbufu.

Nikaelekezwa kwamba, kuna maeneo mawili. Eneo la kwanza limetengwa kwa ajili ya waandishi wenye accreditations za Fifa wale ambao wanatambulika kwa ajili ya kuripoti haya mashindano. Eneo lao lipo uwanjani na watakuwa wakifanya kazi zao pale.

Kuna eneo jingine limetengenezwa katikati ya mji ‘Journalists House’ hapa pameandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari ambao hawakubahatika kupata accreditations za Fifa kuja hapa Urusi kuripoti haya mashindano. Ni tofauti na fainali za kombe la dunia zilizopita, fainali zilizopita mwandishi ambaye hana accreditation ya Fifa alikuwa haandaliwi eneo maalum.

Ukifika hapa  St. Petersburg unakuta facilities zote kwa ajili ya kufanya kazi lakini.

MAWASILIANO

Kingine ni ile campaign ya ‘The City is Ready’ kwa maana ya kwamba mji upo tayari kwa ajili ya kukaribisha wageni na kwa upande wao wanaona kama watalii na zimetwngenezwa call centres maalum zinazoruhusu lugha 5 tofauti, Kirusi, Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani  na Kihispaniola.

Kwa hiyo ukiwa hapa hautapata kikwazo kwa upande lugha pindi utakapo taka kuwasiliana kwa kuwasiliana.

USAFIRI

Kwa upande wa mambo ya usafiri, mashabiki wakishafika airport, vituo vya mabasi na train wanakuta usafiri wa bure ‘shuttles’ kuwapeleka uwanjani na kuwarudisha na vituoni.

Kuna taratibu zingine maalum za kufunga hivi vituo vinavyotoa huduma za kijamii lakini katika msimu huu wa kombe la dunia kutakuwa na tofauti kidogo train, mabasi yatatoa huduma kwa muda zaidi lengo likiwa ni kuhakikisha watazamaji wa wote wa kombe la dunia wanapata huduma bora.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad