Sija-du na Mwanaume Yeyote Nina Mwaka Sasa Tangu Mei Mwaka Jana - Victoria Kimani

Tangu Mei Mwaka Jana Sija-du na Mwanaume Yeyote- Victoria Kimani
HITMAKER wa Ngoma ya China Love ambaye ni Mkenya lakini makazi yake yapo nchini Nigeria, Victoria Kimani amesema kuwa hali ya upweke inamsumbua na kwamba hadi sasa ametimiza mwaka bila ‘kudu’ na mwanaume.


Victoria aliposti kipande cha video katika mitandao yake ya kijamii na kusema;“Huu ni mwezi gani tupo nao? Tangu Mei mwaka jana sija-du na mwanaume yeyote. Kwa hiyo nani ameshindwa? Ni mimi? Au ni wanaume. NI ngumu. Ni kama tupo kwenye ongezeko la joto duniani,” alisema Victoria.

Victoria alikuwa akitoka kimapenzi na prodyuza wa video nchini Nigeria, Stanley Obiamalu ambapo uhusiano wao uliisha Mei, mwaka jana.

Top Post Ad

Below Post Ad