Sikumbuki ni Mimba Ngapi Nimewahi Kutoa- Gigy Money

Sikumbuki ni Mimba Ngapi Nimewahi Kutoa- Gigy Money
Msanii wa muziki Bongo na video vixen, Gigy Money amesema aliwahi kutoa mimba kutokana hakuwa na uwezo wa kulea.

Gigy Money ambaye amejizolea umaarufu mkubwa mtandaoni amesema hayo kupitia Kikaangoni, EATV.

“Sikumbuki ni mimba ngapi nimewahi kutoa ila sio ufahari kusema. Sikuwa na uwezo wa kulea lakini sasa hivi nazaa na nina mpango wa kuanzisha timu ya mpira kupitia watoto wangu”, amesema Gigy Money.

Katika hatua nyingine Gigy Money anaoneka kurudiana na mpenzi wake Mo J baada ya drama za hapa na pale za hivi karibuni.

Utambuka baada ya Gigy Money kujifungua alidai kuwa baba wa mwanae si mpenzi wake (Mo J) ambaye alikuwa anajulikana na wengi kitu ambacho kilileta mshtuko, huku akitupa lawama zake nyingi kwa mpenzi wake huyo kuwa alikuwa hamjali kwa lolote.

Top Post Ad

Below Post Ad