Simba Kucheza na Gor Mahia Fainali Kombe la SportPesa

Simba Kucheza  na Gor Mahia Fainali Kombe la SportPesa
Mabingwa wa ligi ya Tanzania bara Simba wametinga fainali ya michuano ya Super Cup ya kampuni ya Sportspesa baada ya kuwacharaza Kakamega Homeboyz wa Kenya kwa mikwaju 5-4 ya penalti.

Watakutana na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Kenya Gor Mahia ambao wameibuka washindi kwa kuwanyuka Singida FC wa Kenya 2-0.

Mshindi wa mashindano hayo atasafiri hadi England kutoana jasho na Everton katika uwanja wao wa Goodison Park mwezi wa saba.

Bingwa mtetezi Gor Mahia ndiyo iliyocheza na Everton mwaka jana jijini Dar es Salaam ikapoteza kwa mabao 2-1, wafungaji wa Everton wakiwa ni mchezaji nyota wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney na Kieran Dowell, naye Jacques Tuyisenge akaipa Gor Mahia bao lao moja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad