Siwezi Kuruhusu Wanangu Wachezwe Unyago- Shilole

Siwezi Kuruhusu Wanangu Wachezwe Unyago- Shilole
Msanii wa Bongo Flava, Shilole amejibu iwapo ataruhusu wanae wa kike kuchezwa unyago.

Muimbaji huyo akipiga stori na Break ya Clouds TV amesema kuwa ingawa katika kabila lao (Wanyamwezi) wana utamaduni huo hawezi kuruhusu kwa wanae.

“Siwezi, sasa hivi hatuna watu wakubwa ambao wapo, sinaunajua zinakuwaga kama familia. Lakini zamani mambo hayo ndio yalikuwepo tofauti na sasa,” amesema Shilole.

Licha ya kufanya muziki na kujiingiza katika biashara mbali mbali hadi kufungua mgahawa wake, Shilole ni mama wa watoto wawili wa kike.

Top Post Ad

Below Post Ad