Spika Ndugai awatupia dongo Upinzani, awapongeza CCM


Spika Ndugai awatupia dongo Upinz
Spika wa Job Ndugai amewapongeza wabunge kwa kuipitisha Bajeti ya Serikali 2018/19 ya ya Sh 32.45 trilioni kwa kura 266 za wabunge, huku ikiwa imepingwa kwa kura 82 za hapana ambapo amewananga upinzani kwa kushindwa kutoa maoni mbadala ndani ya bunge. 

Akizungumza baada ya zoezi la kutangaza kura kumalizika Ndugai amesema kuwa licha ya kuweza kupitisha bajeti hiyo lakini bado wamefanya kazi kubwa ya kuwachachafya  mawaziri huku wabunge wa upinzani wakishindwa kutoa maoni yao. 

"Hongereni sana, kwani mmewachachafya kweli kweli mawaziri, haswa upande huu, maana upande huu mwingine wao waligoma kutoa maoni yao kwa sababu hawajaandikiwa. Mheshimiwa Silinde siku ile alitoa kali sana. Ni matumaini yetu kwamba wakati ujao watawaandikia hivyo tutapata maoni mbadala," Ndugai. 

Ameongeza "Ndiyo upande wa huku mlisusia kutoa maoni mbadala ya bajeti, maana hata maoni pia ya kesho hamna". 

Pamoja na hayo Ndugai amewakumbusha mawaziri kuwakumbuka wale walioitisha bajeti kwani wasipofanya hivyo wakati mwingine wapitishaji bajeti wataweza kukasirika kisha wakashindwa kupata pesa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad