Sugu ‘Ang’ang’ania’ Mambo ya Magereza...... Aitaka Serikali Kuwalipa Mafao Yao Wastaafu wa Magereza

Sugu ‘Ang’ang’ania’ Mambo ya Magereza......  Aitaka Serikali Kuwalipa Mafao Yao Wastaafu wa Magereza
Mbunge wa Mbeya Mjini, (Chadema) Joseph Mbilinyi (Sugu) ameitaka Serikali kuwasaidia askari magereza wanaostaafu kulipwa mafao bila ya usumbufu kwani wanapostafu husubiri hadi zaidi ya miaka miwili.

Akizungumza leo Juni 4 bungeni, Sugu amesema Serikali huwasumbua askari hao bila sababu za msingi wakati wanafanya kazi ngumu ya kuwatunza wahalifu.

“Mheshimiwa spika, serikali inasema kuhusu askari hawa ambao wamekuwa wakisumbuliwa kutolipwa stahiki zao baada ya kustaafu wakati polisi wanaotukamata na kutupiga wanalipwa mapema lakini wahalifu wote wanarundikwa magereza kwa hiyo hawa wanakuwa na kazi ngumu,” amesema Sugu.

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuwa swali hilo licha ya kuwa ni refu lakini ameamua kuliacha lijibiwe kwani limeulizwa na mtu mzoefu kuliko maswali mengine yanayoulizwa kwa ubabaishaji.

Akijibu swali hilo na swali la msingi kutoka kwa mbuge wa Viti Maalum Lucy Mlowe (Chadema), Naibu Waziri wa Fedha Dk Ashatu Kijaji amesema Serikali inalipa mafao kwa wastaafu wote bila ya upendeleo na kuwa katika kipindi cha hivi karibuni, zililipwa jumla ya Sh 282 bilioni kwa wastaafu mbalimbali.

Naibu waziri amewaondoa hofu pia watumishi wote walioajiriwa katika miaka ya 1980 kupitia Serikali Kuu lakini wakati ule hapakuwa na makato ya mfuko wa kijamii.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad