Tanzania Yaongoza Barani Afrika Kuwa na Wanyama Wengi

Tanzania Yaongoza Barani Afrika Kuwa na Wanyama Wengi
Imeelezwa kuwa jitihada za serikali za kulinda rasilimali za nchi na ushirikiano kutoka kwa wananchi zimesababisha ongezeko kubwa la idadi ya wanyama pori na kuifanya nchi ya Tanzania kuwa nchi yenye wanyama wengi barani Afrika.

Hayo yamebainishwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 29, 2018 katika hotuba yake aliyoitoa Bungeni wakati wakuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge Jijini Dodoma na kusema ili kuitumia vema fursa ya kuwa na vivutio vingi ikiwemo wanyamapori wengi na kuleta tija kwa nchi, serikali itaendelea kuandaa utambulisho wa Tanzania Kimataifa (Destination Branding), lengo likiwa ni kuitambulisha Tanzania kama kituo mahsusi cha utalii duniani.

"Tunalenga kuvutia wageni wa kimataifa waje kuitembelea Tanzania, kuongeza wigo wa kutangaza vivutio na kufanya vivutio vya utalii vifahamike duniani. Pia, serikali inakamilisha mchakato wa kuanzisha Channel maalum kwa ajili ya kutangaza utalii", amesema Waziri Majaliwa.

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu amesema maandalizi ya kuanzisha studio ya kutangaza utalii kwa njia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yanaendelea vizuri, ambapo studio hiyo itawezesha kutambua, kufuatilia na kuwasiliana moja kwa moja na watu wanaofuatilia Tanzania na vivutio vyake.

Top Post Ad

Below Post Ad