Tanzania yaporomoka viwango FIFA
0
June 08, 2018
Tanzania imeshuka nafasi tatu katika viwango vya soka vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la soka duniani (FIFA), huku timu ya Taifa ya Ujerumani ikiendelea kuwa kinara katika msimamo huo na nchi ya Tonga imeshika nafasi ya mwisho kwa dunia.
Katika orodha iliyotolewa leo Juni 7, 2018 na FIFA, imeonesha Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 137 mpaka 140, na kwa upande wa bara la Afrika, Tanzania ipo nafasi ya 39 huku Tunisia ikiwa kinara Afrika.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, Uganda wameonekana kuongoza licha ya kushuka kwa nafasi nane duniani kwa kushika nafasi ya 82, huku wakifutiwa na Kenya(112), Rwanda(136), Tanzania(140), Burundi (148) na Sudan Kusini (156)
Pamoja na kushika nafasi ya 21 duniani lakini Tunisia ni namba moja kwa Bara la Afrika wakifuatiwa na Senegal ambapo kidunia wapo nafasi ya 27, Jamhuri ya kidemokrasia Kongo (38), Morocco (41), Misri (45) Ghana (47), Nigeria (48), Cameroon (49) Burkina Faso (52) na Mali (64) zipo 10 bora na Somalia ikishika nafasi ya mwisho.
Bara la Ulaya, limeendelea kuongoza ambapo nchi saba zimefanikiwa kutinga 10 bora ya mataifa bora duniani wakiongozwa na Ujerumani aliyeshika na nafasi ya kwanza na nafasi ya pili imekwenda kwa Brazil wakifuatiwa na Ubelgiji, Ureno, Argentina, Uswisi, Ufaransa, Poland, Chile na Hispania walioshika nafasi ya 10.
Tags