Tofauti kati ya Eid ul-Fitr na Eid ul-Adha


Waumini wa dini ya Kiislamu kote duniani wanasherehekea sikukuu ya Eid ul-Fitr. Hii ni moja ya sikukuu za idi? Baadhi ya watu, hasa wasio wamini wa dini hiyo wamekuwa wakikanganyikiwa kati ya Eid ul-Fitr na Eid ul-Adha. 

Lakini hizi ni sikukuu tofauti 

Eid ul-Fitr 
Eid ul-Fitr maana yake ni "sikukuu ya kumaliza mfungo" na kutumiwa kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. 

Siku hii huwa ni siku rasmi ya mapumziko katika mataifa mengi yenye waumini wengi wa Kiislamu. Hata hivyo idadi ya siku za mapumziko huwa tofauti katika nchi mbalimbali. 

Waislamu huanza sherehe hizi kwa kukusanyika kwa maombi ya kila mwaka ambayo hufanyika muda mfupi baada ya macheo. 


Ni kawaida kuwaona Waislamu wakikusanyika katika misikiti na viwanja vya wazi kwa maoni ya pamoja. 

Kabla ya ibada hiyo, huwa wanatoa sadaka kwa maskini (huitwa Zakat) ambayo ni moja ya nguzo kuu katika dini ya Kiislamu. 

Ni kawaida kwa miji mikuu mataifa ya Kiislamu kupambwa sana na sherehe kubwa kuandaliwa, watoto kununuliwa nguo mpya na kupewa zawadi mbalimbali. 

Siku hii huadhimishwa baada ya kuonekana kwa mwezi wa Shawwal, Mwezi huu ulionekana Alhamisi jioni katika baadhi ya mataifa yakiwemo ya Afrika Mashariki na uarabuni. 

Ndio maana sikukuu ya Eid ul-Fitr inaadhimishwa leo Kenya, Uganda na Tanzania nan chi kama vile Qatar, UAE, Saudi Arabia, Indonesia, Uturuki, Morocco, Algeria, Tunisia, Libya na Malaysia wanasherehekea Eid leo. 

Mwezi haukuonekana India na Pakistan Alhamisi hivyo wao watasherehekea Eid ul-Fitr Jumamosi Juni 16 sawa na New Zealand na Australia. 

Eid ul-Adha 
Eid al-Adha ndiyo sikukuu kuu zaidi ya kidini miongoni mwa Waislamu kote duniani na pia huwa ni siku ya mapumziko mataifa mengi yenye Waislamu. 

Nchini Kenya Eid ul-Fitr huwa ni siku ya mapumziko lakini Eid ul-Adha huwa si siku ya mapumziko ya taifa miaka yote. 

Eid al-Adha maana yake ni "sikukuu ya kutoa kafara" kwa Kiarabu na hutumiwa kukumbuka wakati nabii Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ishmael alivyoamriwa na Allah, lakini akapewa kondoo na Mungu amtoe kafara badala yake. 

Sikukuu ya Eid ul-Adha huadhimishwa kuanzia siku ya 10 tangu kuonekana kwa mwezi wa Dhu al-Hijjah. 

Ibada ya Hajj kwenda Mecca huanza siku mbili kabla ya Eid al-Adha na tarehe yake huthibitishwa baada ya kuoenakana kwa mwezi huo wa Dhu al-Hijjah. 

Eid al-Adha ina majina mbalimbali katika mataifa ya Kiislamu: 


Eid el-Kabir nchini Nigeria na MoroccoTabaski nchini Senegal na Gambia.Kurban Bayrami nchini UturukiHari Raya Haji nchini Indonesia, Malaysia na Singapore.Eid è Qurbon, nchini Iran.
Bakr-Id or Qurbani Eid, nchini India, Bangladesh, na kwa Kiurdu pia. 
Waislamu pia huvalia mavazi yao mazuri na ya kupendeza siku hii na huenda msikitini kwa maombi. 

Baadhi humchinja ng'ombe, mbuzi au kondoo kukumbuka kitendo cha imani cha nabii Ibrahimu. 

Hula chakula chenye nyama na huwapa jamaa, majirani na maskini nyama ya mnyama waliyemchinja. 

 Katika baadhi ya mataifa na miji hairuhusiwi watu kuwachinja wanyama kwao nyumbani hivyo vichinjio hutumiwa. Waislamu pia hutoa pesa za hisani kipindi hicho. 

Waislamu hutumia Eid ul-Adha kusherehekea utiifu kamili wa nabii Ibrahimu kwa amri ya Mungu na kuwakumbusha wenyewe kuwa tayari kutoa kafara chochote ili kutimiza maagizo ya Mungu na kumfuata. 

Eid Mubarak 
Eid Mubarak kwa Kiarabu maana yake ni "sherehe au sikukuu njema au yenye Baraka". 

Ni salamu za kawaida wakati wa sikukuu za Eid, Wakati wa Eid ul-Fitr, salamu nyingine maarufu ni 

Ciid wanaagsan - Somalia.Mutlu Bayramlar - Uturuki.Selamat Idul Fitri - Indonesia.Selamat Hari Raya - Malaysia, Brunei, na Singapore.Barka da Sallah - baadhi ya maeneo ya Nigeria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad