Kumekuwa na maneno makali kutoka kwa Rais Donald Trump kuelekea mkutano wa mataifa tajiri G7 unaotarajiwa kufanyika nchini Canada na, kwamba inatoza ushuru mkubwa kwa bidhaa zitokazo Marekani na kusabisha mazingira magumu yasiyoenda na sera za kifedha.
Kitendo cha Trump kuongeza ushuru katika bidhaa za chuma kumemuweka katika mazingira ya kutofautiana na mataifa wanachama wa G7.
Akizungumza awali na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau mjini Ottawa, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliwaambia waandishi wa habari kwamba watatumia mkutano ujao wa G7 kumshawishi rais Trump dhidi ya msimamo wake kibiashara.
Nitarudia kumwambia rais Trump kwamba hatua alizochukua hazina manufaa hata kwa uchumi wa taifa lake. Kwa mimi hili ni jambo lililowazi, huwezi kuanzisha vita vya kibiashara na washirika wako.
Sisi sote tunashirikiana katika mzozo wa Syria na Iraq na maeneo mengine duniani.
Ni washirika na tunabadilishana taarifa, majeshi yetu yanashirikiana kulinda uhuru wetu.
Katika mazingira ya kimataifa tunayokabiliana kwa siku za leo hatuwezi kuanzisha vita vya kibiashara miongoni mwetu.
Nitajaribu kumshawishi kurejea katika hali ya kawaida kibiashara na kuondoa hali hii ya hofu kibiashara."Anasema Macron.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ni rais wa pili Afrika kulakiwa na Donald Trump Marekani
Hata hivyo Macron amesisitiza kuwa bado muungano wao unaweza kusonga mbele hata bila Marekani kama italazimika kuwa hivyo.
" Labda Rais Trump hajali kuhusiana na kujitenga kwake, lakini hatujali tupo tayari hata kuwa mataifa sita, kama itabidi kwa sababu mataifa hayo sita yanawakilisha umoja wetu na hadhi yetu yenye manufaa kwa mujibu wa historia ya muungano huu na dunia ya sasa."ameongeza Macron
Hatua ya hivi karibuni ya Rais Trump ya kuongeza ushuru kwa bidhaa za washirika wake imezua mzozo mpya wa kibiashara.
Trump Atoa Maneno Makali Kuelekea Mkutano wa Mataifa Tajiri G7
0
June 08, 2018
Tags