Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo baada ya watumiaji wa mabasi hayo kupata huduma ya bila malipo tangu Juni 3 hadi leo Juni 4, 2018 na kusema imefanya hivyo kwa lengo la kutoathiri shughuli za abiria hao.
"Tunatambua kusafirisha abiria bila ya kulipa nauli kuna sababisha hasara kubwa kwa kampuni lakini kwa kuzingatia umuhimu wa abiria wetu kupata huduma na hadhi ya taifa, hasara iliyopatikana haiwezi kuzidi madhara ambayo yangetokea kwa kusimamisha huduma", amesema Bugaywa.
Pamoja na hayo, Bugaywa ameendelea kwa kusema "kutokufika kwa wahudumu kwenye vituo kwa siku mbili mfululizo kumetokana na kucheleweshewa mishahara ya mwezi Aprili na Mei ambayo awali ilikuwa inalipwa na UDART kupitia Maxcom. Lakini badala ya mkataba huo kuisha na wakati tukisubiri kamati zilizoundwa na wakala anayesimamia mradi DART Agency, kusimamia na kukabidhi mfumo kwa UDART.
Kampuni iliomba taarifa za benki za wafanyakazi hao ili waweze kulipwa mishahara moja kwa moja kutoka UDART, bahati mbaya hil halikuwezekana hadi sasa tumefikia hatua hii".
Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa amewahakikishia abiria wa mfumo huo na wananchi kwa ujumla kuwa mradi huo ni muhimu kwa ustawi wa taifa na kwa namna yeyote hawapo tayari kuhatarisha uendelevu wake kwa manufaa mapana ya taifa.