Kambi ya Upinzani Bungeni imetaja mambo matano ambayo ni vipaumbele kwa bajeti mbadala ya mwaka wa fedha 2018/19.
Vipaumbele hivyo ni elimu, kilimo, viwanda katika mnyororo wa thamani ya kilimo, huduma za afya, maji na uchumi.
Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe alisema hayo jana Juni 16, 2018 jijini Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari.
“Vipaumbele hivi ukivitengea fedha za kutosha mathalan hizi Sh700 bilioni za Stigler’s Geoge kwa mwaka mmoja tu, maisha ya wananchi yangekua, lakini si kwa kuweka kipaumbele katika maeneo yasiyokuwa na tija moja kwa moja kwa wananchi,” alisema.
Mbowe alikosoa bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19 ya Sh32.5 trilioni iliyowasilishwa bungeni Juni 14, 2018 akisema haitekelezeki.
Kiongozi huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema, amlisema Serikali imekuwa haizingatii sheria ya fedha na kinachotengwa sicho kinachotolewa na hasa fedha za maendeleo