Ukimwi na Mimba Vilinisumbua Sana- Gigy Money

Ukimwi na Mimba Vilinisumbua Sana- Gigy Money
Msanii na 'video vixen’ maarufu nchini, Gift Stanford 'Gigy Money’ amesema kuwa katika vitu vilivyowahi kumtesa akilini kwake wakati wa ukuaji wake ni pamoja na nasaha za mama yake kuhusu kujikinga na maambukizi ya UKIMWI pamoja na mimba za utotoni.

Gigy amefunguka hayo kupitia KIKAANGONI ya East Africa Television, inayorushwa mubashara kwenye ukurasa wake wa Facebook, ambapo amesema alipopevuka mama yake alimwambia kuwa kuna mimba na UKIMWI anatakiwa kujiepusha na vishawishi.

''Nilipopevuka tu mama yangu akaniambia kuna Mimba na UKIMWI hivyo vitu vilinisumbua sana lakini vilinisaidia'', amesema Gigy Money.

Gigy amesema kuwa vitisho hivyo vilimsaidia, ambapo kwa sasa ametimiza umri wa miaka 21, akiwa mzima wa afya na amefanikiwa kujifungua mtoto wake kawaida.

Top Post Ad

Below Post Ad